Nahodha wa Uholanzi Robin van Persie, akiwa mazoezini. |
Wapo Wenyaji Brazil, ambao ni Mabingwa
wa Dunia mara 5, wapo Mabingwa wengine wa zamani France, Germany na
Argentina lakini pia zipo timu ambazo hazijawahi kutwaa Kombe hili
ambazo ni Colombia, Belgium, Netherlands na Costa Rica.
JE NI TIMU ZIPI 4 ZITASONGA NUSU FAINALI?
PATA TATHMINI/DONDOO FUPI:
+++++++++++++++++++++++++
KOMBE LA DUNIA
ROBO FAINALI
Ijumaa Juni 4
1900 France v Germany
2300 Brazil v Colombia
Jumamosi Juni 5
1900 Argentina v Belgium
2300 Netherlands v Costa Rica
+++++++++++++++++++++++++
FRANCE v GERMANY
Hili ni pambano murua la Vigogo wa Ulaya waliowahi kutwaa Kombe la Dunia.
Kwenye Fainali hizi huko Brazil, France
wameng’ara na kutandika Bao kibao wakati Germany wameonyesha kudorora na
walipata shida kubwa kuitoa Algeria Raundi iliyopita wakionyesha Soka
lisilotulia hasa kwenye ushambuliaji.
Gotze, Ozil na Muller Siku zote huwa
hatari wakipewa nafasi kwenye maeneo ya kushambulia lakini huko Brazil
wameonyesha kupata taabu sana kuzipenya Difensi zilizojilundika.
Lakini dhidi ya Algeria, alipoingizwa Schurle badala ya Gotze aliepwaya, Germany walionekana kupata kasi na kuwa hatari mno.
Hata hivyo, tatizo kubwa la Germany ni
Difensi yao ambayo hukaba kwa kusogea mbele na kukaribia mstari wa kati
na hilo husababisha kupenywa na mara nyingi Kipa wao huwaokoa kwa
kucheza kama ‘Beki Mfagiaji’.
Kwenye Mechi hii, wanakutana na France
ambayo ni hatari katika kushambulia na tayari wana Goli 10 katika Mechi 4
za Mashindano haya.
Walipocheza na Nigeria na kumwingiza Griezmann na Benzema kusogea na kucheza kama Straika wa kati walionekana kuwa hatari mno.
Wakicheza hivyo, na hasa wakiwaanzisha Griezmann na Valbuena, basi Difensi ya Germany itapata shida sana.
VIKOSI VINATARAJIWA:
France: Lloris; Debuchy, Koscielny,Varane, Evra; Sissoko, Valbuena, Matuidi, Pogba; Griezmann, Benzema
Germany: Neuer; Höwedes, Hummels, Mertesacker, Boateng; Schweinsteiger, Lahm, Kroos; Götze, Özil, Müller
BRAZIL v COLOMBIA
Hii
ni Mechi baina ya Nchi za Bara la Marekani ya Kusini na inawakutanisha
Wenyeji Brazil , ambao ni ni Mabingwa wa Dunia mara 5, na Colombia
ambayo safari hii ni Timu inayong’ara mno huku Straika wao James
Rodriguez akimeremeta na kuongoza kwa ufungaji Mabao akiwa na Bao 5.
Kwenye Mashindano haya Brazil
wameshindwa kuzitawala baadhi ya Mechi zao kama ilivyotarajiwa na
wamekabiliana na upinzani mkali mno.
Brazil wameonyesha wazi kumtegemea mno
Neymar huku wakikosa Sentafowadi mkali kwenye umaliziaji na mwenye uchu
wa kufunga kwani Fred, na hata akiingizwa Jo kumbadili, ubutu na udhaifu
wa kufunga ulikuwa ukionekana dhahiri.
Lakini tofauti na matarajio, Difensi ya
Brazil imesimama imara kuliko mashambulizi yao na wanapaswa kubadili
mfumo wao wakicheza na Colombia ambayo imeonyesha Soka safi kupita Timu
nyingi.
Hili ni pambano la kuvutia na, ingawa
baadhi ya Wachambuzi wanaipa matumaini Colombia hasa kwa Soka lao na
ukali wa James Rodriguez kwa kucheka na nyavu, lakini itakuwa ni ujinga
wa hali ya juu kuipuuza Brazil ambao ni Wenyeji na pia umwamba wao
Duniani si kitu kigeni.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil: Cesar; Alves, Silva, Luiz, Marcelo; Fernandinho, Paulinho; Willian, Oscar, Neymar; Fred
Colombia: Ospina; Zuniga, Zapata, Yepes, Armero; Aguilar, Sanchez; Cuadrado, James Rodriguez, Ibarbo; Gutierrez
ARGENTINA v BELGIUM
Huu ni mtanange.
Argentina, kama walivyo jirani zao
Brazil, ndio wanapewa nafasi kubwa kubeba Kombe la Dunia lakini hadi
sasa uchezaji wao umekuwa chini ya kiwango.
Ingawa Lionel Messi amekuwa akipachika Magoli, uchezaji wake umekuwa chini na hadi sasa hawajakutana na Timu kali hasa.
Dhidi ya Timu dhaifu, Iran na Bosnia,
Messi amekuwa akikabwa na kunyimwa nafasi na hilo kumvunja moyo na
uchezaji wake kudidimia kiasi.
Argentina na Belgium itakutanisha Timu
yenye vipaji dhidi ya Timu yenye uwezo mkubwa kiufundi na hili itaifanya
Mechi iwe ngumu mno hasa kwa vile Belgium ina Wachezaji wenye miguvu.
Kwenye Difensi Belgium wako imara lakini
wana udhaifu wa kushindwa kudhibiti mashambulizi ya kustukiza na ya
haraka wakati Argentina wana udhaifu mkubwa kwenye ngome yao na
wanamtegemea mno Mascherano kupokonya Mipira toka kwa Wapinzani.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Argentina: Romero, Zabaleta, Fernandez, Garay, Rodriguez, Mascherano, Di Maria, Gago, Messi, Higuain, Lavezzi
Belgium: T. Courtois, Alderweireld, Van Buyten, Kompany, Vermaelen, Witsel, Fellaini, Mertens, De Bruyne, Hazard, Origi
NETHERLANDS v COSTA RICA
Wengi hawakutegemea Costa Rica kufikia hatua hii na Mechi hii itakutanisha Mastraika hatari dhidi ya Difensi imara.
Netherlands, wakiongozwa kwenye
mashambulizi na Arjen Robben, Robin van Persie na Wesley Sneijder,
wamepachika Bao 12 katika Mechi 4 za Fainali hizi.
Lakini Costa Rica, kwenye Mechi 4 huko
Brazil, wamefungwa Bao 2 tu licha ya kuzivaa Timu kali zikiwemo England,
Italy na Uruguay.
Licha ya kuwa na Difensi imara, Costa
Rica pia ina Wachezaji wazuri kwenye mashambulizi ambao ni Joel
Campbell, Mchezaji wa Arsenal, na Bryan Ruiz, na hawa wakiachiwa tu ni
wepesi kufunga.
Kocha wa Netherlands, Louis van Gaal,
alionyesha umahiri wake kwa kubadili mbinu Uwanjani wakati wa Mechi
kwani kwenye Raundi iliyopita, huku wakiwa nyuma Bao 1-0 na Mexico,
alimtoa Nahodha wake Robin van Persie na kumwingiza Jan Klaas Huntelaar
ambae ndie aliewafungia Bao la Pili na la ushindi kwa Penati ya Dakika
ya 94 baada ya Sneijder kuwasawazishia katika Dakika ya 88.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Netherlands: Cillessen, Verhaegh, Kuyt, Vlaar, De Vrij, Janmaat, Blind, Wijnaldum, Sneijder, Van Persie, Robben
Costa Rica: Navas, Gamboa, Umana, Gonzalez, Miller, Diaz, Tejeda, Borges, Ruiz, Campbell, Bolanos
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
ROBO FAINALI IJUMAA, JULAI 4, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
France v Germany [57] |
ROBO FAINALI |
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro |
2300 |
Brazil v Colombia [58] |
ROBO FAINALI |
Estadio Castelão, Fortaleza |
JUMAMOSI, JULAI 5, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
Argentina v Belgium [59] |
ROBO FAINALI |
Nacional, Brasilia |
2300 |
Netherlands v Costa Rica [60] |
ROBO FAINALI |
Arena Fonte Nova, Savador |
NUSU FAINALI JUMANNE, JULAI 8, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61] |
NUSU FAINALI |
Estadio Mineirão, Belo Horizonte |
JUMATANO, JULAI 9, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Mshindi 59 Mshindi 60 [62] |
NUSU FAINALI |
Arena Corinthians, Sao Paulo |
MSHINDI WA TATU JUMAMOSI, JULAI 12, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62 |
MSHINDI WA 3 |
Nacional, Brasilia |
FAINALI JUMAPILI, JULAI 13, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2200 |
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62 |
FAINALI |
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro |
0 comments:
Post a Comment