- Dogo mnene lazima awe Golikipa
- Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.
- Penalti itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.
- Mechi itaisha kama kila mchezaji atakua amechoka au giza likiingia.
- Penati ni hatua 6 na zinapimwa na mchezaj wa timu inayopigiw penati(Mara nying anakuw mrefu ili point ya penati iwe mbal).
- Kama haushiriki kwenye kutengeneza mpira ulipofumuka unaweza usipate namba uwanjani.
- Mkicheza kwa dau muwe makin na mshika hela anawez kupotea muda wowote, hasa timu yake inapofungwa.
- Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka,au kutungua mpira endapo utanasa kwenye mti huku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.
- Mwenye mpira akikasirika,mechi ndo itakua imefika mwisho.
- Inaruhusiwa kubadili golikipa kama penalti ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.Pia ukikosa penati jiandae kwa kipigo.
- Messi wa timu hatoi pasi, anatembea na mpira mwanzo mwisho na anaweza kufany hivy mechi nzima wengine mkabak mnakimbia tu.
- Mwenye mpira huwa hatolewi hata akicheza vibaya.. Hakuna refa,faulo n makubalian ya pande mbili; mchezaji anaweza kuzunguka na mpira hata nyuma ya goli.
- Uwanja ni popote, ila game husimama akipita mtu mkubw, (shikamoo nyingii.)
- Faulo siyo suala la refa bali la kisasi, ukikatwa na wewe kata!
mpya
nyumbani
TUKUMBUSHANE SHERIA 14 ZA BOLI TULIPOKUWA WADOGO:
12:10 PM
No Comments
0 comments:
Post a Comment