UHOLANZI YASUBIRI MATUTA KUITOA COSTA RICA.

UHOLANZI imetinga Nusu Fainali kwa ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana na Costa Rica ndani ya dakika 120 usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Dunia nchini Brazil.
Baada ya timu yake kupelekeshwa kwa dakika 120 na Costa Rica na kushindwa kupata bao, kocha Louis van Gaal alimuingiza kipa wa Newcastle, Tim Krul kwa ajili ya penalti.
Krul alipasha misuli yake moto haraka na kwenda kumbadili Jasper Cillessen dakika ya 118, kisha akaedna kuokoa penalti mbili kuipelekea nchi yake Nusu Fainali ya michuano hiyo.

Super sub: Holland's Tim Krul makes the decisive save to deny Costa Rica's Michael Umana in the shoot-out
Kaseja wao: Kipa wa Uholanzi, Tim Krul akipangua penalti ya nne ya Costa Rica iliyopigwa na Michael Umana na kuipeleka Uholanzi Nusu Fainali

Krul aliokoa penalti ya pili ya Costa Rica  iliyopigwa na mchezaji wa Fulham, Bryan Ruiz na ya nne iliyopigwa na Michael Umana.
Raha zaidi ni kwamba, Nahodha Robin van Persie, Wesley Sneijder, Arjen Robben na Dirk Kuyt wote wakafunga penalti zao na sasa Uholanzi itakutana na Argentina katika Nusu Fainali ‘tamu sana’ yenye hadhi hata ya fainali.
Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen/Krul, dk120, De Vrij, Vlaar, Martins/Huntelaar dk105, Kuyt, Wijnaldum, Sneijder, Blind, Robben na van Persie, Depay/Lens dk76. 
Costa Rica: Navas, Gamboa/Myrie dk78, Acosta, Diaz, Gonzalez, Ruiz, Borges, Tejeda/Cubero dk97, Bolanos, Campbell/Urena dk66 na Umana. 

Credit:Bongostaz.

0 comments:

Post a Comment