BOLT AWEKA REKODI MPYA JUMUIYA YA MADOLA



 Huyu jamaa ni nomaa! Usain Bolt ameisaidia Jamaica kuweka rekodi nyingine ya dunia ya mita 100 katika relay, maarufu kama relay 4 x 100 (kupokezana vijiti). Rekodi aliyoweka ni sekunde 37.58.


Katika mchuano huo mkali kwenye Jumuiya ya Madola, Bolt alilazimika kurekebisha mambo baada ya mwenzake aliyekimbia katika nafasi ya tatu kuchelewa kumkabidhi kijiti.
Huku mpinzani wake kutoka England akiwa mbele yake, Bolt alipiga kasi ya aina yake na kumvuja hadi kuweka rekodi hiyo.
Ingawa michuano inafanya Scotland ambako England ni ndugu zao, lakini mashabiki waliripuka kwa furaha kutokana ushindi huo wa Bolt uliokuwa na msisimko. England walishika nafasi ya pili na Trinidan&Tobago wakashika ya tatu.



0 comments:

Post a Comment