STARS, WAMBURA OUT.






Taifa Stars imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa mara nyingine tena.
Kwa mara ya pili mfululizo inatolewa na Msumbiji baada ya kufungwa mabao 2-1.
Katika mechi hiyo mjini Maputo, wenyeji walipata bao lao katika dakika ya 45 mfungaji akiwa Josemar.

Kipindi cha pili, Stars walisawazisha katika dakika ya 77 kupitia Mbwana Samatta.
Baada ya hapo, mashambulizi yalikuwa ya zamu na kila upande ukionyesha kupania kushinda.
Stars ndiyo walikuwa wakihitaji ushindi zaidi wakati Msumbiji wangevuka hata kwa sare ya bao 1-1 baada ya ile sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam.
Elias Pelembe, mchezaji ambaye amekuwa akiionea Taifa Stars, alifunga bao la pili katika dakika ya 84.
Pelembe maarufu kama Domingues ndiye alimaliza kazi hiyo na sasa Stars imeng’olewa kwa jumla ya mabao 4-3.
Mara ya mwisho, Stars iling’olewa kwenye michuano hiyo mjini Maputo kwa changamoto za mikwaju ya penalti baada ya sare ya mabao 1-1 Dar na Maputo.

Katika Hatua nyingine: wanachama 860 wa Simba hapo jana wamemfuta na kumfukuza aliyekuwa mgombea wa Urais wa klabu hiyo Michael Richard Wambura.
Pamoja na Wambura, wanachama hao wamepitisha uamuzi wa kuwafukuza uanachama wenzao wengine 72.

Uamuzi huo umefikiwa kwenye mkutano wa wanachama wa Simba uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment