CHELSEA YANG'ARA MBELE YA LEICESTER CITY

MSHAMBULIAJI Diego Costa ameendelea kung’ara Chelsea baada ya jioni hii kuiwezesha The Blues kushinda mechi ya pili mfululizo Ligi Kuu ya England kwa kuichapa Leicester City mabao 2-0 Uwanja Stamford Bridge.
Costa alifunga bao la kwanza dakika ya 62, kabla ya 
Eden Hazard kufunga la pili dakika ya 77. Diego Costa alimpisha mkongwe Didier Drogba dakika ya 80 huku akipigiwa makofi wakati anatoka nje.
Diego Costa ameendelea kung'ara Chelsea akifunga katika ushindi wa 2-0 leo 

Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Oscar/Willian dk70, Hazard, Schurrle/Ramires dk64 na Costa/Drogba dk80.
Leicester City; Schmeichel, De Laet, Konchesky, Morgan, Hammond/Taylor-Fletcher dk73, King, Schlupp, Mahrez/Albrighton dk68, Nugent na Ulloa/Wood dk84.

0 comments:

Post a Comment