Liverpool sasa imehamia kwa mshambuliaji
nyota wa Cameroon mkongwe, Samuel Eto’o.
Kocha wake, Brebdan Rodgers ameona anaweza
kumnasa ili kuziba pengo la Luis Suarez aliyekwenda Barcelona.
Rodgers alifanya juhudi za kumnasa Lois Remy
lakini akafeli vipimo vya afya.
Kocha huyo wa Liverpool, imeelezwa Eto’o ni
chaguo la kwanza na akikwama, badi Wilfred Bony anayekipiga Swansea atakuwa
namba mbili.
Bonny anakipiga katika kikosi cha timu ya
taifa ya Ivory Coast na alifunga bao la nne wakati Tembo walipoifunga Taifa
Stars mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, yeye akifunga la nne dhidi ya kipa
Juma Kaseja.
0 comments:
Post a Comment