ARSENAL WABEBA NGAO YA HISANI

Taji la mapema: Wachezaji wa Arsenal wakifurahia Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Manchester City 3-0 Uwanja wa Wembley, London jioni ya leoGetting a soaking: The triumphant Arsenal players sprayed each other with champagne afterwards
Oxlade-Chamberland, Wilshere, Cazorla, Sanchez na Arteta kwa raha zao 

ARSENAL imebeba Ngao ya Jamii baada ya kuwafumua mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City mabao 3-0 jioni hii Uwanja wa Wembley, London.
Katika mchezo huo wa kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya England, mabao ya The Gunners yamefungwa na Santi Cazorla dakika ya 21, Aaron Ramsey dakika ya 42 na Olivier Giroud dakika ya 60.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy, Chambers, Koscielny/Monreal dk46, Gibbs, Arteta, Sanchez/Oxlade-Chamberlain dk46, Ramsey/Campbell dk86, Wilshere/Flamini dk68, Cazorla/Rosicky dk70 na Sanogo/Giroud dk46.
Man City: Caballero, Clichy, Boyata, Nastasic, Kolarov/Richards dk76, Navas/Sinclair dk85, Toure/Milner dk60, Fernando, Nasri/Silva dk46, Dzeko/Zuculini dk60 na Jovetic.

0 comments:

Post a Comment