KOCHA
Louis Van Gaal leo ameiongoza Manchester United katika mchezo wa tatu
mfululizo Ligi Kuu ya England bila kushinda, licha ya kumuanzisha
mchezaji mpya, Angel de Maria aliyemsajili wiki hii kutoka Real Madrid
kwa Pauni Milioni 59.7.
United imetoka safe ya bila kufungana na timu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, Burnley Uwanja wa Turf Moor, hivyo ikikusanya pointi mbili katika tatu baada ya awali kufungwa 2-1 na Swansea Uwanja wa Old Trafford na kulazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland Uwanja wa Light.

![]() |
Di Maria akiwa kazini hapo jana |
Angel di maria akipasua katikati ya wachezaji wa Burnley leo
![]() |
Di Maria akimpisha Anderson baada ya kushindwa kuifungia Man United |
Van
Gaal alimpumzisha mchezaji huyo aliyeweka rekodi ya kusajiliwa kwa
fedha nyingi zaidi kihistoria Uingereza dakika ya 70, nafasi yake
akichukua Anderson. Aliwapumzisha pia Juan Mata dakika ya 87 akiingia
Adnan Januzaj na Robin van Persie dakika ya 73 akiingia Dany Welbeck.
Kikosi cha Man United kilikuwa; De Gea, Jones, Evans, Blackett, Young, Fletcher, Di Maria/Anderson dk70, Mata/Januzaj dk87, Valencia, Rooney na Van Persie/Welbeck dk73.
Burnley; Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Mee, Arfield, Jones, Marney, Taylor/Reid dk88, Ings/Barnes, dk78 na Jutkiewicz.

0 comments:
Post a Comment