MSHAMBULIAJI
Diego Costa, ameendelea kung’ara Chelsea baada ya leo kufunga mabao
mawili katika ushindi wa 6-3 dhidi ya Everton Uwanja wa Goodison Park
Ligi Kuu ya England.
Costa alifunga sekunde ya 35 na dakika ya 90, wakati mabao mengine ya The Blues yalifungwa na Branislav Ivanovic dakika ya tatu, Coleman akajifunga dakika ya 67, Nemanja Matic dakika ya 74 na Ramires dakika ya 77.
Samuel
Eto’o aliifunga timu yake ya msimu uliopita inayofundishwa na kocha
Mreno Jose Mourinho dakika ya 76, wakati mabao mengine ya Everton
yamefungwa na Mirallas dakika ya 45 na Naismith dakika ya 69.
Kipa wa Everton, Tim Howard alinusurika kulimwa kadi nyekundu baada ya kudakia mpira nje ya eneo la penalti.
Kikosi
cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta,
Ramires, Matic, Willian/Mikel dk75, Fabregas/Drogba dk89, Hazard/Luis
dk83 na Costa.
Everton:
Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas,
Naismith, McGeady/Eto'o dk70 na Lukaku/Besic dk89.
![]() |
Diego Costa kulia ameendelea kufanya vizuri Chelsea |
0 comments:
Post a Comment