WINGA
Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja, Argentina
ikilipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa kuifunga 4-2 Ujerumani usiku huu
katika mchezo wa kirafiki mjini Dusseldorf, Ujerumani.
Mchezaji
huyo ghali zaidi kuwahi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima
alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla
ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika
muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil.
Mabao
matano kati ya sita yamefungwa na wachezaji wa Ligi Kuu ya England,
huku Andre Schurrle akiifungia Ujerumani kabla ya Gotze kuwafungia bao
la pili mabingwa hao wa dunia. 
Kifaa halisi; Angel di Maria ameng'ara vilivyo leo Argentina ikilipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa Ujerumani
CREDITS:BONGOSTAZ.COM
0 comments:
Post a Comment