![]() | |
Nahodha babu kubwa; Wayne Rooney akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee usiku huu(BONGOSTAZ) |
mpya
ulaya
ROONEY AIBEBA ENGLAND.
9:33 PM
No Comments
NAHODHA
wa England, Wayne Rooney ameitendea haki beji katika mchezo wake wa
kwanza tangu arithi mikoba ya Steven Gerrard aliyestaafu, baada ya
kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway Uwanja wa
Wembley usiku huu.
Nahodha
huyo wa Manchester United pia, alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa
penalti dakika ya 68, kufuatia nyota wa Liverpool, Raheem Sterling
kuchezewa rafu kwenye eneo la penalti.
Katika
mchezo huo uliohudhuriwa na watu 40,181 – idadi ndogo zaidi ya
mahudhurio kwenye Uwanja wa Wembley tangu ufunguliwe tena, kinda
Sterling alizawadiwa heshima ya mchezaji bora mechi baada ya kazi nzuri
kwenye kikosi cha Roy Hodgson usiku huu.
0 comments:
Post a Comment