Utamu wa mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Simba dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Jumamosi umezidi kuongezeka.
Utamu
huo umezidi baada ya Gor Mahia kueleza kwamba mashabiki wake wakiwa
kwenye mabasi matano wanaondoka Nairobi kuja Dar es Salaam kuishangilia
timu yao katika mechi hiyo hiyo dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa.
"Kweli wanakuja wakiwa kwenye mabasi matano, hivyo watawapa wakati mgumu mashabiki wetu, lazima wajiandae.
"Mashabiki
wa Gor Mahia hushangilia mwanzo mwisho na wanajulikana kama mashabiki
namba moja nchini Kenya," alisema Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey
Nyange 'Kaburu'.
Hiyo
itakuwa ni mechi ya kwanza ya Simba ya kirafiki ya kimataifa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa chini ya Patrick Phiri kwa
mara nyingine.
Simba imekuwa kambini kisiwani Unguja ambako imecheza mechi tatu na kushinda zote.
Mechi yake ya mwisho dhidi ya KMKM, ilishinda kwa mabao manne huku ikionyesha soka safi na la kuvutia.
0 comments:
Post a Comment