CHELSEA YAIUA MARIBOR 6-0:DRODBA AFUNGA: ANGALIA VIDEO NA PICHA HAPA.


Chelsea 6-0 Maribor: Drogba & Hazard strike in Blues rompDidier Drogba amefunga goli lake la kwanza tangu arudi Chelsea katika ushindi mnono wa magoli 6-0 walioupata Chelsea dhidi ya Maribor katika ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne huko Stamford Bridge.

Chelsea ambao walizanza kampeni za kusaka ubingwa huo kwa sare na Schalke 04 ya Ujerumani, walionekana kuwazidi wapinzani wao kwa sehemu kubwa.
Maribor ambao walikuwa na rekodi ya kutokufungwa katika mechi 8 za UEFA Champions kujumuisha na ushindi mmoja na sare mbili katika kundi lao walionekana kuchanganywa na pasi na kasi ya Chelsea.


Chelsea walipata uongozi dakika ya 13 wakati mchezaji wake Loic Remy alipopata mpira kutoka kwa Terry kisha akaingia ndani na kupiga shuti lililoingia upande wa chini wa kulia mwa goli la Maribor, Remy hata hivyo hakudumu mpaka mwisho baada ya kupata majeraha ambayo yalimfanyaatolewe na kuingia Drogba.
Drodba ndiye aliyeiandikia goli la pili Chelsea baada ya kupiga penati nzuri iliyomuhamisha kipa wa Maribor baada ya Ales Mertel kushika mpira eneo la hatari.

Goli la tatu la Chelsea lilfungwa na Terry, huku l ne likifungwa na Viler wa Maribor baada ya shuti la Hazard kumgona dakika ya 54,

Maribor walipata penati lakini wakaikosa baada ya Ibarimi kupiga shuti lililogonga mwamba. 

Magoli mengine yalifungwa na Hazard dakika ya 77 na 90 na kufanya jumla ya ushindi kuwa 6-0.

0 comments:

Post a Comment