Goli la Sergio Arguero dakika la 29 liliwapa uongozi Man City, na dakika ya 38 Milner aliiongezea City goli la pili.Mpaka mapumziko CSKA Moscow 0-2 Man City.
Hata hivyo baada ya mapumziko mambo hayakwenda sawa kwa Man City ambapo dakika ya 64 Seydou Doumbia aliifungia CSKA goli la kwanza. Kukiwa kumebaki dakika 4 mchezo kumalizika kitumbua cha Man City kiliingia mchanga baada ya CSKA kuzawadiwa penati baada ya Aleksandar Kolarov kumchezea rafu laini Ahmed Musa wa CSKA.
Natkho aliifungia goli CSKA kupitia mkwaju huo wa penati a kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo.
0 comments:
Post a Comment