ESSIEN AMEPATA EBOLA?


Essien posted to his Instagram account to dispell the rumours he had contracted the Ebola virus
Kiungo wa timu ya taifa ya Ghana na Ac Milan ya Italia Michael Essien amekanusha taarifa zilizosambaa tangu juzi kwenye mitandao kuwa amepata virusi vya Ebola,

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mcezaji huyo amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo na walioandika ni waandishi 'Makanjanja'. Baadae mchezaji huyo alipost picha iliyomuonesha akitabasamu na mwenye afya.


Klabu ya Ac Milan pia nayo haikuwa nyuma kukanusha habari hizo ambapo imetoa taarifa ikisema kuwa hakuna ukweli kuhusu taarifa hizo na hakuna msemaji wake aliyeongea na mtandao wowote kuhusu habari hizo kama ilivyodaiwa na wavumishaji hao.

Kumekuwa na tabia inayokua ya uvumishaji wa taarifa za uongo hasa kuwaelekea wanamichezo ambapo huu umekuwa ni uvumi mkubwa baada ya ule uliodai kuwa bingwa wa uzito wa juu zamni Mike Tyson amebadili jinsia.

0 comments:

Post a Comment