
Mabingwa mara 24 wa ligi kuu ya Tanzania bara, Yanga leo hii wameingina kambini katika hoteli ya Landmatk iliyopo ufukweni katika bahari ya hindi,jijini Dar es salaam, hali hiyo ni tofauti na kile kilichopendekezwa awali na viongozi wa timu huku habari za ndani zikiripoti kuwa maamuzi hayo yamefanywa na kocha wa timu hiyo mbrazil Marcio Maximo.
Taarifa zaidi zimedai kuwa Maximo alipendekeza kambi hiyo isifanyike Zanzibar ili kuwapa wachezaji muda wa kutosha wa kufanya mazoezi na kutowachosha kwa safari za mbali.
Kwa sasa Yanga watakuwepo katika hoteli hiyo na kufanyia mazoezi katika uwanja wa Boko Basihaya ambao unamilikiwa na Maveterani wa Boko, huku ikidaiwa kuwa Yanga wameukodi uwanja huo kwa gharama za shilingi 350,000/= kwa siku na watautumia mpaka siku ya ijumaa.
0 comments:
Post a Comment