Liverpool hawapaswi kumpa Raheem Sterling £100,000 kwa wiki.

Mkongwe wa Liverpool John Aldridge anaamini Mshambuliaji Sterling anapaswa kupewa mkataba mnono zaidi ya £100,000 kwa wiki anazolipwa sasa. Mshambuliaji huyo ambaye ameshika vichwa vya habari katika klabu kubwa Ulaya zikiwapo Real; Madrid na PSG. Sterling amekuwa msaada mkubwa kwa kikosi cha Liverpool kwa kipindi cha takribani miezi 12 iliyopita akifunga magoli 9 katika mechi 33. . Umuhimu wa Sterling umeongezeka hasa baada ya Luis Suarez aliyekuwa tegemeo la safu ya ushambuliaji kuhamia Barca kwa ada ya Pauini Milioni 75. Aldridge anaamini Sterling anastahili mkataba mpya kumpongeza kwa kiwango chake, pia akishauri Klabu inatakiwa kutafuta namna tofauti za kumuongezea morali mchezaji huyo. "Katika Umri huu mdogo kama ule Sterling hatakiwi kufikiria mikataba na pesa" alinukuliwa Aldridge akiongeza "Sterling alitakiwa kufikiria kuhusu kucheza mpira na kufahia". "Inatakiwa Liverpool wampe mkataba ambao una manufaa ili kumuongezea Morali"

0 comments:

Post a Comment