Neymar alifungua kalamu ya mabao dakika ya 18 kwa shuti kali la mguu wa kulia akiwa akiwa kati kati ya box baada ya kupata pasi kutoka kwa Diego Tardelli, dakika ya 48 Neymar aliindikia timu yake bao la pili kwa shuti la chini upande wa kulia wa goli, shukrani kwa msaada wa Philippe Coutinho.
Dakika ya 65 Robinho aliingia kumbadili Diego Tardelli, Brazil. Kakáakaingia badala ya ElÃas na Souza akambadili Luiz Gustavo katika dkika ya 73 hali iliyowaoneze nguvu Brazil na kuongeza mashambulizi langoni kwa Japan yaliyozaa matunda dakika ya 77 mfungaji akiwa Neymar,Neymar alihitimisha kalamu yake ya magoli dakika ya 81 ya mchezo kwa goli safi la kichwa akimalizia kazi ya Kaka na kufanya matokeo kuwa 4-0 mpaka mwisho wa mchezo.
Kwa matokeo hayo Neymar amefikisha magoli 40 katika meci 58 alizocheza katika timu hiyo y taifa na ameingia katika rekodi mpya ya kukaa namba tano katika list ya wachezaji waliofunga magoli mengi katika kikosi cha Brazil kwa muda wote, namba 1 ikikaliwa na mkongwe Pelle mwenye magoli 77.
LIST YA WAFUNGAJI BORA WA BRAZIL:
1. Pele - 772. Ronaldo - 62
3. Romario - 55
4. Zico - 48
5. Neymar - 40
6. Bebeto - 39
0 comments:
Post a Comment