Daley Blind amefunga goli lake la kwanza tangu kuanza kuichezea Manchester United na kuisaidia kupata sare ya 2-2 dakika za mwisho na kupona kipigo kutoka kwa West Brom.
West Brom ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga dakika ya 8 baada ya Stephane Sessègnon kumalizia pasi ya Andre Wisdom kwa shuti kali lililotinga kona ya juu ya goli.
Goli hlo lilidumu hadi mapumziko ambapo kipindi cha pili kocha Va Gaal alimtoa Ander Herrera na kumuingiza Marouane Fellaini, ambaye mchango wake ulionekana na dakika ya 48 alifanikiwa kuisawazishia timu yake kwa kumalizia pasi ya Di Maria kwa kifua.
Hata hivyo furaha ya Man U haikudumu kwani dakika ya 66 West brom walikuwa mbele tena kwa goli la Saido Berahino aliyefunga baada ya counter attack.
Katika dakika ya 87 ikionekana Man U wamesahpoteza mchezo shujaa wao Daley Blind aliisawazishia timu yake hiyo na kuipa ahueni ya kuondoka na point 1.
0 comments:
Post a Comment