Manchester United wanaingia uwanjani wakiwa wameshinda michezo miwili
mfululizo ikiwemo mchezo dhidi ya West Ham 2-1, Everton 2-1.
West Bromich wanaingia uwanjani wakiwa kwenye fomu nzuri ila tu
hawana rekodi nzuri na michezo ya nyumbani dhidi ya Manchester United,
katika michezo 18 ya mwisho West Bromich ameweza kufungwa michezo 13.
Manchester United itaingia uwanjani huku ikimkosa nahodha wao Wayne
Rooney kwa sababu ya kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu,upande
mwingine wachezaji Chris Smalling Ander Herrera, Ashley Young, Phil
Jones and Michael Carrick wameendelea kufanya mazoezi leo na wachezaji
wenzao kwa maandalizi ya mchezo wa leo.
0 comments:
Post a Comment