BAO
pekee la Sergio Aguero jioni hii limeipa ushindi mwembamba wa 1-0
Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad
dhidi ya mahasimu, Manchester United.
Aguero
alifunga bao hilo dakika ya 63 akimfunga kipa wa United, David de Gea
ambaye timu yake ilichea pungufu tangu dakika ya 39, baada ya Chris
Smalling alipotolewa kwa kadi nyekundu. Beki mwingine wa United, Marcos Rojo alitolewa nje kwa machela baada ya kuumia bega.
Kikosi
cha Manchester City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis,
Clichy, Navas, Toure, Fernando, Milner/Nasri dk70, Aguero/Fernandinho
dk83 na Jovetic/Dzeko dk71.
Manchester
United: De Gea, Valencia, Smalling, Rojo/McNair dk56, Shaw, Fellaini,
Blind, Rooney, Januzaj/Carrick dk43, Van Persie/Wilson dk82 na Di
Maria.
0 comments:
Post a Comment