Klabu ya Entente Satif kutoka Algeria imeshinda ubingwa wa kilabu
bora barani Afrika kwa mara ya kwanza katika miaka 26 baada ya kuishinda
klabu ya AS Vita Club kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutokana
na mabao ya ugenini kufuatia sare ya 3-3 siku ya jumamosi.
Raundi ya pili ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini
Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika
mechi ya kwanza iliochezwa mjini Kinshasa.
Setif ilianza kuona lango na wapinzani wao dakika nne katika kipindi
cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye alifunga bao kupitia pasi ya El
Hadi Belameiri.
Lakini wageni hao walisawazisha dakika tano baadaye kupitia Lema
mabidi aliyepiga mkwaju kutoka nje ya eneo la kupigia penalti ili
kuimarisha matumaini ya timu yake.
Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.
Bao hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha
mchezo mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia
mbinu chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka
mchezo huo kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.
0 comments:
Post a Comment