MBEYA
City imeendelea kufanya vibaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga.
Kwa matokeo hayo, Mbeya City inabaki mkiani mwa Ligi Kuu baada ya kuambulia pointi tano katika mechi sita, maana yake iko hatarini kushuka daraja.

Malimi
Busungu aliifungia bao la kwanza Mgambo JKT dakika ya 11 kwa penalti
kufuatia Nassor Gumbo kukwatuliwa na Hassan Mwasapili katika eneo la
hatari na refa Israel Nkongo wa Dar es Salaam akatoa adhabu hiyo.
Mgambo ambayo wikiendi hii itacheza na Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilipata bao lake la pili dakika ya 24 kupitia kwa Ally Nassor, kabla ya kiungo wa zamani wa Simba SC, Steven Mazanda kuifungia bao la kufutia machozi dakika ya 76.
Mbeya City ilikuwa timu tishio msimu uliopita baada ya kupanda tu Ligi Kuu, kiasi cha kumaliza katika nafasi ya tatu, nyuma ya Yanga SC na Azam FC, lakini msimu huu imepoteza makali.

credit: BONGOSTAZ.
0 comments:
Post a Comment