Timu zote hizi znatinga kwenye mpambano
huu wakitoka kwenye Mechi ngumu ambapo France walipelekwa puta na
Nigeria na hatimae kushinda na Germany kusota na kuifunga kwa mbinde
Algeria.
Huko Brazil, France wameonekana kung’ara
ukilinganisha na Germany ambao walianza vizuri kwa kuicharaza Portugal
4-0 lakini wamekuwa wakififia Mechi hadi Mechi lakini tatizo kubwa la
Germany ni Difensi yao ambayo hukaba kwa kusogea mbele na kukaribia
mstari wa kati na hilo husababisha kupenywa na mara nyingi Kipa wao
Neuer huwaokoa kwa kucheza kama ‘Beki Mfagiaji’.
Kwenye Mechi hii, wanakutana na France
ambayo ni hatari katika kushambulia na tayari wana Goli 10 katika Mechi 4
za Mashindano haya.
Walipocheza na Nigeria na kumwingiza Griezmann na Benzema kusogea na kucheza kama Straika wa kati walionekana kuwa hatari mno.
Wakicheza hivyo, na hasa wakiwaanzisha Griezmann na Valbuena, basi Difensi ya Germany itapata shida sana.
Uso kwa Uso
Germany na France zimekutana mara 25 na France kushinda 11 Germany 8 na Sare 6.
VIKOSI VINATARAJIWA:
France: Lloris; Debuchy, Koscielny,Varane, Evra; Sissoko, Valbuena, Matuidi, Pogba; Griezmann, Benzema
Germany: Neuer; Höwedes, Hummels, Mertesacker, Boateng; Schweinsteiger, Lahm, Kroos; Götze, Özil, Müller
REFA: Nestor Pitana [Argentina]
RATIBA
**Saa za Bongo
ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
France v Germany [57] |
ROBO FAINALI |
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro |
0 comments:
Post a Comment