Brazil wanatinga kwenye Robo Fainali
wakitokea kwenye Mechi ngumu waliyokwenda Sare 1-1 na Chile katika
Dakika 90, ikabaki 1-1 baada Dakika 120 na hatimae kushinda kwa Penati
3-2 huku Supastaa wao Neymar akimaliza Gemu hii akiwa na maumivu kibao.
Kwenye Mechi na Colombia Brazil
watamkosa Kiungo Mkabaji wao Luiz Gustavo ambae yupo Kifungoni Mechi 1
kwa kuzoa Kadi za Njano mbili.
Colombia wanatinga kwenye Mechi hii
wakitoka kuinyuka Uruguay Bao 2-0, Bao zote zikifungwa na Chipukizi wao
wa Miaka 22, James Rodriguez, anaechezea AS Monaco huko France na ambae
ndie anaongoza kwa Mabao kwenye Fainali hizi za Kombe la Dunia akiwa na
Bao 5.
Kwenye Mashindano haya Brazil
wameshindwa kuzitawala baadhi ya Mechi zao kama ilivyotarajiwa na
wamekabiliana na upinzani mkali mno.
Brazil wameonyesha wazi kumtegemea mno
Neymar huku wakikosa Sentafowadi mkali kwenye umaliziaji na mwenye uchu
wa kufunga kwani Fred, na hata akiingizwa Jo kumbadili, ubutu na udhaifu
wa kufunga ulikuwa ukionekana dhahiri.
Lakini tofauti na matarajio, Difensi ya
Brazil imesimama imara kuliko mashambulizi yao na wanapaswa kubadili
mfumo wao wakicheza na Colombia ambayo imeonyesha Soka safi kupita Timu
nyingi.
Hili ni pambano la kuvutia na, ingawa
baadhi ya Wachambuzi wanaipa matumaini Colombia hasa kwa Soka lao na
ukali wa James Rodriguez kwa kucheka na nyavu, lakini itakuwa ni ujinga
wa hali ya juu kuipuuza Brazil ambao ni Wenyeji na pia umwamba wao
Duniani si kitu kigeni.
Uso kwa Uso
Timu hizi zimekutana mara 25 na Brazil kushinda mara 15 Colombia 2 na Sare 8.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil: Cesar, Marcelo, Silva, Alves, Luiz, Paulinho, Fernandinho, Hulk, Neymar, Fred, Willian.
Colombia: Ospina; Armero, Yepes, Zapata, Zunjiga; Guarin, Sanchez, Vargas, Martinez, Rodriguez; Teofilo.
REFA: Carlos Velasco [Spain]
RATIBA
**Saa za Bongo
ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014 |
|||
SAA | MECHI | KUNDI | UWANJA |
2300 | Brazil v Colombia [58] | ROBO FAINALI | Estadio Castelão, Fortaleza |
0 comments:
Post a Comment