UJERUMANI NUSU FAINALI-UFARANSA KWA HERI

UJERUMANI imeweka rekodi kwa kufuzu Nusu Fainali ya kombe la Dunia mara ya nne mfululizo baada ya jioni hii kuilaza Ufaransa bao 1-0 Uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro, Brazil.
Shujaa wa Ujerumani leo alikuwa ni beki Mats Hummels aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 12 akimalizia kazi nzuri ya Toni Kroos.
Pamoja na kufungwa, Ufaransa leo walicheza nyuma ya bahati, kwani walipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga mabao hususan dakika za mwishoni za mchezo huo. 
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa; Lloris, Debuchy, Varane, Sakho/Koscielny dk72, Evra, Valbuena/Giroud dk85, Pogba, Cabaye/Remy dk73, Matuidi, Griezmann na Benzema. 
Ujerumani: Neuer, Lahm, Hummels, Boateng, Howedes, Ozil/Gotze dk83, Kroos, Schweinsteiger, Khedira, Muller na Klose/Schurrle dk69. 
Mkali wa leo: Beki wa Ujerumani, Mats Hummels akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao pekee timu yake katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Dunia Uwanja wa Maracana, Brazil dhidi ya Ufaransa na kuiwezesha kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment