Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya amethibitisha uteuzi wa kocha huyo wa zamani wa Uganda, Cranes katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Nairobi Hotel.
Wanasoka wa zamani wa kimataifa wa Kenya, Mussa Otieno na Simon Mulama pia wameteuliwa kuwa Wasaidizi wa kocha huyo na Meneja.
Mzoefu Afrika Mashariki; Bobby Williamson alifanya vizuri akiwa na Uganda na sasa anahamishia mafanikio hayo Kenya |
Jukumu la kwanza la Mscotland huyo litakuwa ni kutetea Kombe la Mataifa ya Afrika Mashaiki na Kati, CECAFA Challenge Novemba mwaka huu.
Kocha huyo aliingia Afrika Mashariki Agosti mwaka 2008 alipopewa jukumu la kuifundisha Uganda Cranes ambako alidumu kwa miaka mitano kabla ya kuhamia Gor Mahia Julai 5 mwaka 2013.
Bobby anachukua nafasi ya Adel Amrouche aliyefukuzwa baada ya Kenya kushindwa kuingia kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco, kwa kutolewa na timu dhaifu, Lesotho.
0 comments:
Post a Comment