KLABU ya Manchester City imethibitisha usajili wa kiungo wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard kwa mkopo wa miezi sita.
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England wametangaza habari hiyo leo, na Lampard
alifanya mazoezi na timu yake mpya kwa mara ya kwanza baadaye leo.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 36 amesajiliwa na klabu dada ya Manchester
City, New York City kama mchezaji huru, lakini anarudi England kwa
sababu msimu wa Ligi Kuu ya Marekani unaanza mwakani.
Siku
ya kwanza: Frank Lampard amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza na
Manchester City leo baada ya kukamilisha usajili wake wa mkopo kutoka
New York City
Rangi
mpya: Kiungo wa zamani wa Chelsea amefanya mazoezi Uwanja wa Carrington
na wachezaji wenzake wa timu yake mpya, Manchester City
0 comments:
Post a Comment