WADHAMINI
wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Vodacom wametoa kezi zinazofanana kabisa kwa
mahasimu wa jadi nchini, Simba na Yanga SC- tofauti ni moja tu, rangi.
Katika
hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu za Ligi Kuu msimu mpya leo, Vodacom
wamekabidhi jezi za rangi ya kijani na njano kwa Yanga na nyekundu na
nyeupe kwa Simba, lakini muundo ni mmoja kila kitu.
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) liliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya
Mashindano, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alihakikisha timu zote 14 za
Ligi Kuu zinapatiwa vifaa hivyo.
Timu zote 14 zilituma wawakilishi wao katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam.
Ligi
Kuu inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu, mabingwa watetezi, Azam
FC wakifungua dimba na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,
Dar es Salaam.
Yanga
SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro siku hiyo, wakati washindi wa tatu, Mbeya City
wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20.
Mechi
nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United
watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga,
Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na
Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi
mkoani Pwani.
Mabingwa
wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC wataanza kampeni ya kutwaa tena taji
hilo Septemba 21 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi
hiyo itatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumapili wiki
hii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga SC.
0 comments:
Post a Comment