UONGOZI
wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi
ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake,
Emmanuel Okwi kuwa huru.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa
na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Mapande
amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko
yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na
malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema
kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo
haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
![]() |
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga SC, Sam Mapande kulia akizungumza na Waandishi wa Habari leo. Kushoto ni Msaidizi wake, Onesmo Mpinzile. |
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema
kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata
malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi
kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za
usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa
kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslahi.

credits: Bin zubeiry.
0 comments:
Post a Comment