AZAM VS MBEYA CITY HAPATOSHI


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Azam leo wameanza safas\ri asubuhi na basi lao jipya kuelekea Mbeya kwa ajili ya mpambano mkali wa ligi kuu katika uwanja wa Sokoine siku ya Jumamosi hii.

Azam wameondoka wakiwa na kikosi cha wachezaji 20, huku afisa habari wa Azam Jaffer Idd amewataja wachezaji ambao hawajaondoka sababu bado hawajawa fiti ni Bocco, Friday na Mwantika ambao sasa wameanza mazoezi mepesi, Domayo naye pia ameanza kujifua na goti limeanza kukunja lakini Kimwaga yeye bado kabisa.

Azam wameamua kuondoka mapema leo ili wapate siku za kupumzika na vile vile kufanya maandalizi ya mwisho na kuzoea mazingira.

Mabingwa hao watashuka uwanjani wakiwa na pointi saba na wako katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakati nafasi ya nne inashikiliwa na wenyeji hao Mbeya City.

Credits:Kandanda.

0 comments:

Post a Comment