Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Argentina na timu ya
Manchester City ya Uingereza Sergio Kun Aguero amekuwa mwiba katika
mchezo wa leo baada ya kufunga mabao 4 peke yake na kuipatia ushindi
timu yake Manchester City wa mabao 4-1.
Sergio Aguero alikuwa wa kwanza kupachika bao dakika ya 13 ya mchezo
na kunako dakika ya 15 tu Christian Eriksen alisawazisha na kufanya
mabao kuwa 1-1.Mchezo ulizidi kuwa mkali huku Manchester City kuonekana
wakisaka ushindi kwa nguvu na ndipo tena Sergio Aguero akapachika bao la
pili kwa njia ya penalty katika dakika ya 32.Kipindi cha pili Spurs
walipata penalty na nafasi ya kusawazisha ila Roberto Soldado alikosa
penalty.Dakika ya 67 ya mchezo Federico Fazio mlinzi wa Spurs alionyesha
kadi nyeku na kuadhibiwa penalty kuelekea upande wao na si mwingine
tena Sergio Aguero akapachika bao la 3 kwa timu yake.Tottenham walizidi
kupotea mchezoni huku Manchester City kuonekana bado kutoridhika na
mabao hayo na kwa mara nyingine dakika ya 75 Sergio kuzamisha jahazi la
Tottenham kwa kupachika bao 4 kwa timu yake Manchester City.
Hadi filimbi ya mwisho Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4 huku Tottenham Spurs wakiambulia bao 1.
0 comments:
Post a Comment