MATOKEO EPL: CHELSEA YANG'ARA, ARSENAL CHUPUCHUPU, SAUTHAMPTON 8-0 SUNDERLAND.

Ligi ya Ungereza imeendelea tena wiki hii kwa michezo mingi na viwanja tofauti huku vinara wa ligi hiyo kwa sasa Chelsea wamezidi kujichimbia kileleni baada ya kuwachapa Crystal Palace kwa mabao 2-1.

Chelsea walianza kwa moto sana na kuweza kupata bao la mapema mnamo dakika ya 6 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao Oscar.Dakika ya 40 mlinzi wa Chelsea Ceser Azpilicueta alipata kadi nyekundu sambamba na Damien Delaney mlinzi wa Crystal Palace nae alipata kadi nyekundu baada ya mwanzo kuwa na njano moja.Mpaka mapumziko Chelsea walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 huku timu zote wakicheza wakiwa 10.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Chelsea wakionekana kuwa bora na kusaka ushindi,jitihada zao zilizaa matunda baada ya kiungo wao mwenye kiwango cha juu sana Cesc Frabregas kupachika bao la 2 kwa Chelsea,Chelsea walizidi kutawala mpira kwa asimia kubwa sana ila dakika ya 90 ya mchezo Crystal Palace walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Fraizer Campbell.

Matokeo mengine katika ligi hiyo ni Washika bunduki wa London Arsenal nusu kudondokea pua katika uwanja wa nyumbani baada ya kupata sare ya 2-2 dhidi ya Hull City,Southampon wamefanya kufuru kubwa baada ya kuibuka na ushindi wa rekodi ya mabao 8-0 dhidi ya Sunderland,Everton 3-0 Aston 
Villa,Newcastle 1-0 Leicester City,Burnley 1-3 West Ham na Manchester City 4-1 Totten Ham Spurs.

0 comments:

Post a Comment