Katika mchezo huo kila timu iliingia uwanjani kwa presha kubwa ya
kupata ushindi dhidi ya mwenzake,huku timu ya Simba ikiingia uwanjani na
kipa namba tatu na chipukizi Manyika kutokana na kuumia kwa makipa wao
Ivo Mapunda na Casillas,Manyika alionekana kuwa bora zaidi katika mchezo
huo na kushangaza watu uwanjani uwanjani kwani hawakutegemea kumuona
akiwa katika ubora huo.
Kipindi cha kwanza cha mchezo Simba walionekana kuwa bora zaidi huku
mshambuliaji Okwi akionekana kuwa mwiba katika nafasi ya ulinzi ya
Yanga.Kipindi cha pili cha mchezo huo mambo yalikuwa kinyume baada ya
Yanga kurudi mchezoni na kuonekana kuwa bora zaidi ya Simba ila ubora
wao uliishia hivyo hivyo hawakuweza kupata bao lolote.
Hadi kipenga cha mwisho cha mchezo matokeo yalibaki kuwa 0-0.
CREDIT:SALEH JEMBE/ KANDANDA TZ.
0 comments:
Post a Comment