Sababu za kocha Pep Guardiola kundoka Barca na Kwenda Bayern zimewekwa wazi ambapo imeelezwa kuwa mpango wa kuondoka Barca ulikuwa mgumu na wa muda mrefu kwa Pep ambapo kabla ya kuongea na Klabu Guardiola aliongea na marafiki zake kuwashirikisha uamuzi huo.
Sababu kubwa ya kwanza imedaiwa ni kuishiwa mbinu za kukifundisha kikosi cha Barca ambapo kwa mtazamo wake aliona hana mbinu mpya ya kukibadili kikosi hicho.
Haikuwa sababu pekee pia;
Sababu nyingine ilidaiwa ni uongozi ambapo katika wakati wake Guardiola alipitachini ya marais wawili tofauti wa kwanza akiwa ni Sandro Rosell na wa pili ni Joan Laporta, wakati wa Sandro Rosell imedaiwa kuwa Guardiola alivumilia mengi licha ya kuwa rais huyo alikuwa mtata ambaye alikuwa ana tabia ya kulipuka kama Volcano, akikuunga mkono katika hili basi dakika moja ijayo atakupinga katika lile.
Katika kipindi hicho Guardiola alishinda mataji yote sita amabayo ni La Liga, Copa del Rey, Champions League,e European and Spanish Supercups naKlabu bingwa ya dunia.
Baada ya Rosell alikuja Laporta ambaye ndiye alikuwepo mpaka Guardiola anaondoka, Laporta alichangia kuondoka kwa Guardiola kwa kuwa alikuwa babe zaidi akiamua kila kitu na kubana uhuru wa maamuzi ya Guardiola kama kocha kuanzia kwenye masuala ya kiufundi, usajili, marupurupu kwa benchi la ufundi na mengineyo, hali iliyomnyima uhuru Guardiola.
Rais huyo mpya ambaye alikuwa hapatani na rais aliyepita alimuona Guardiola kama kibaraka wa mpinzani wake huyo na hivyo kufanya mambo kuwa magumu zaidi.
Sababu nyingine imedaiwa kuwa ni kumchoka kwa wachezaji wake ambao walichoshwa na mazoezi ya muda mrefu hasa ambapo tofauti na mawazo ya kochahuyo, wachezaji walijiona kama mabingwa kwa kuwa tayari walikuwa na makombe mikononi.Guardiola aliwahi kunukuliwa akisema "Nilipoona mwanga unapungua mbele ya macho ya wachezaji wangu, nilijua ndiyo wakati sahihi wa kuondoka.
Kwa upande wake Guardiola ameendelea kusisitiza kuwa sababu kuu ya kuondoka ilikuwa ni kuishiwa mbinu na siyo nyingine zaidi, ingawa ukweli unabaki kuwa hali ya mahusiano katika klabu haikuwa nzuri wakati akiondoka.
0 comments:
Post a Comment