Timu hizo zenye ushindani mkubwa zinakutana zikiwa katika nafasi
tofauti kwenye msimamo wa ligi hiyo unaoongozwa na Mtibwa Sugar mabingwa
wa mwaka 1999 na 2000.
Yanga ambao ndiyo wenyeji katika mchezo huo wa Jumamosi ipo katika
nafasi ya tatu ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili kati
ya tatu ilizo cheza msimu hiyo inatokana na baada ya kupoteza mchezo wa
kwanza dhidi ya vinara Mtibwa Sugar.
Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa na hali mbaya baada ya
kushindwa kupata ushindi katika mechi tatu ilizocheza msimu huu na zote
kuambulia sare na kujikuta ikiwa nafasi ya 10 na pointi zao 3.
Kuelekea kwenye mpambano huo presha imezidi kupanda kwa mashabiki wa
timu zote mbili ambazo mara mechi yao ya mwisho kukutana zilitoka sare
ya kufungana bao 1-1,lakini matokeo ya mechi za hivi karibuni yanaipa
nafasi ya kufanya vizuri Simba ambayo imeanza vibaya msimu huu.
Simba imeweza kutoka sare na timu za Coastal Union,Polisi Moro na
timu ngeni katika ligi ya msimu huu Stand United kibaya zaidi ikiwa
kwenye uwanja wa nyumbani wa taifa Dar es Salaam
Simba inaingia katika mchezo huo tegemeo pekee likiwa kwa
kmshambuliaji wake raia wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye amekuwa na
mchango mkubwa tangu asajiliwe msimu huu akitokea kwa mahasimu wao
Yanga.
Ingawa Okwi hakwenda kwenye kambi ya Afrika ya Kusini lakini kocha
Patrick Phiri,anatarajia msaada mkubwa kutoka kwa Mganda huyo sambamba
na winga Ramadhani Singano na mkongwe Amri Kiemba ambaye Jumapili
iliyopita alionyesha kiwango cha juu na kufunga bao la pili katika
ushindi wa 4-1 kati ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Benin.
Faraja nyingine ya kocha Phiri ni kureja uwanjani kwa kipa wake
chaguo la kwanza Ivo Mapunda aliyekuwa ameumia kidole cha mkono lakini
mshambuliaji mpya Raphael Kiongera na nahodha wa zamani Nassor Masoud
Chollo watakosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeruhi yanayo
wakabili
Tofauti na Yanga ambao kikosi chao kina na ari kubwa ya kupata
ushindi niwazi kitakuwa na lengo la kutaka ushindi katika mechi hiyo ili
kuwafikia Mtibwa Sugar katika uongozi wa Ligi hiyo.
Kocha Marcio Maximo amekuwa na matumaini makubwa katika pambano hilo
ambalo kwakwe litakuwa la kwanza tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo
mwezi Julai mwanzoni
Niwazi Maximo atakuwa akitaka kujiwekea rekodi ya kuifunga Simba na
kupata ushindi wa tatu mfulilizo kwenye mechi za Ligi Kuu kwa sababu
idadi kubwa ya wachezaji wake waliokuwa wagonjwa wamepona na wapotayari
kwa mchezo huo wa leo.
Maximo kwenye sehemu ya ulinzi atakuwa anategemea zaidi ulinzi wa
Nadiri Haroub ‘Cannavaro’Kelvini Yondani huku Oscar Joshua aliyekosa
mechi mbili zilizopita kutokana na maumivu ya paja aliyoyapata kwenye
mechi dhidi ya Mtibwa akitarajia kumtumia baada ya kupona na kuonyesha
kiwango cha juu kwenye mechi ya Taifa Satrs dhidi ya Benin Jumapili
iliyopita.
Na katika safu ya ushambuliaji Yanga itakuwa ikiwategemea zaidi
wachezaji Geilson Santana JAJA,Hamisi Kiiza Andrey Coutinho na Nizar
Khalfani huku safu ya kiungo ikiwategemea zaidi Mnyarwanda Haruna
Niyonzima na Hassani Dilunga ambaye ambao wamekuwa kwenye kiwango cha
juu siku za karibuni.
Kwa kikosi hiki niwazi Maximo atataka vijana wake wacheze kandanda
safi ili kushinda na kufuta uteja wa kufungwa na Simba kwani rekodi
zinaonyesha katika miaka mitano timu hizo zimekutana mara 11 simba
imeshinda mara nn Yanga mara tatu na mara nne zimetoka sare
Lakini kibaya zaidi timu zote mbili zitataka kushinda mchezo huo
kwani mechi zinazofuata wikiendi ijayo zitakuwa ugenini Yanga itakuwa
kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga ilhali Simba itasafiri hadi
Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine kuifuata Tanzania Prisons.
Vipigo vikubwa zaidi ilivyoipata Yanga kutoka kwa Simba bado vipo
kwenye kumbu kumbu za mashabiki wa timu hiyo na wamekuwa na matumaini
makubwa kuwa ari iliyonayotimu yao inaweza kupoza machungu kwa kurudisha
vipigo hivi vya Mei 6 2012 Simba kushinda 5-0 na kile cha Desemba 21
2013 mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo Yanga ilifungwa 3-1 na Simba.
Presha imekuwa kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu zote mbili hususani
wale wa Simba ambao wanakosa furaha kutokana na mwenendo wa timu yao
katika mechi tatu zilizopita na ukilinganisha ubora wa wapinzani wao
Yanga ambao wameonekana kujipanga kulipiza kipigo cha mabao matano na
yale matatu katika mechi ya mtani jembe.
Simba ilikwenda Afrika Kusini Kujiandaa na pambano hilo na wapinzani
wao Yanga walibaki Dar es Salaam wakipiga kambi kwenye Hoteli ya
LandMark kujiandaa na mechi hiyo kila upande umedhamiria kushinda bila
kujali Simba wamesema watazinduka katika mechi hiyo huku Yanga nao
wakitamba kuvunja mwiko kwa kulipa kisasi cha mabao 5-0.
Mwamuzi Israel Nkongo ndiye aliyepewa jukumu la kupuliza kipyenga
katika pambano hilo lakini mwamuzi huyo amekuwa na bahati mbaya na Yanga
kwani alishawahi kupigwa na mchezaji Stevano Mwasika msimu wa
2011.2012,wakati alipokuwa anaichezesha timu hiyo dhidi ya Azam FC
iliyoshinda mabao 3-1.
Nkongo mwamuzi mwenye beji ya FIFA,Shirikisho la soka limekuwa na
imani kubwa na mwamuzi huyo kwamba ataliendesha na kulimaliza salama
pambano hilo na kila upande kuridhika na maamuzi atakayoyatoa kwa dakika
zote 90.
SOURCE:GOAL.COM
0 comments:
Post a Comment