TISHIO LA EBOLA : GHANA AU AFRIKA KUSINI KUIBADILI MORROCO UENYEJI WA AFCON 2015

South Africa or Ghana could replace Morocco as 2015 Afcon hostsUenyeji wa mataifa ya Afrika mwaka 2015 kwa nchi ya Morocco umeingia matatani baada ya nchi hiyo kuiomba CAF kuyaahirisha mashindano hayo kutokana na tishio la kusambaa kwa virusi vya Ebola wakati wa mashindano hayo.
Imedaiwa kuwa Morocco imeiandikia barua CAF kuitaka ihahirishe mashindano hayo na kutishia kujitoa endapo ombi lake halitakubaliwa.
CAF kwa upande wake imelikataa ombi hilo la Morocco na kufanya maskani ya AFCON 2015 kuwa mashakani nchini humo.
Afrika Kusini: CAF imedaiwa kuliandikia barua shirkisho la soka Afrika kusini(SAFA) kuliomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, ingawa shirikisho hilo bado linajadili uwezekano huo na halijathibitisha rasmi.
 Msemaji wa SAFA Dominic Chimhavi amesema hapo jana kuwa Afrika Kusini inaweza kukubali kuandaa mashindano hayo akijinadi kwa ubora wa viwanja na mazingira kwa ujumla ya nchi yake.
"Tunajua kuwa Morocco wameomba kujiondoa katika kuandandaa AFCON 2015 kwa hofu ya ebola......CAF wameichagua Afrika kusini kama sehemu mbadala ya kuandaa mashindano hayo ingawa bado kuna mambo mengi ya kujadili kabla ya kufikia maamuzi ya mwisho" alisema Dominic.

Ghana: Kwa upande wao Ghana kupitia kwa waziri wao wa michezo na vijana Mh.Mahama Ayariga amesema Ghana ni moja ya nhci ambazo CAF wameonesha nia ya kuzipa uenyeji endapo Morocco itashindwa.
"CAF wametuandikia barua siku chache zilizopita na kutuambia kuwa Morocco wameonesha dalili kubwa za kujitoa uenyeji wa mashindano hayo ikiwa CAF haitabadili ratiba ya mashindano hayo" alisema waziri huyo.

0 comments:

Post a Comment