Chama cha mpira cha Nigeria (NFF) kimetangaza kumfukuza kazi kocha wa Super Eagles Stephen Keshi leo. Kufukuzwa kwa kocha huyo mahiri kumekuja baada ya kusindwa kukiongoza kikosi cha Super Eagles vema katika mbio za kucheza fainali za Mataifa ya Afrika(AFCON) mwaka 2015 huko Morocco.
Kibarua cha Kocha huyo kilianza kuwa mashakani tangu mwezi Septemba baada ya Nigeria kufungwa nyumbani magoli 3-2 na Congo,kisha kutoa sare na Afrika Kusini huko Cape Town, na baadae kufungwa na Sudan huko Khartoum.
Ahueni ya Nigeria ilikuja siku ya Jumatanoya jana tarehe 15 oktoba 2014 baada ya kupata ushindi wa kwanza wa magoli 3-1 dhidi ya Sudan ingawa haukotosha kuokoa kibarua cha Kocha huyo.
Baada ya Keshi kutimuliwa Amodu Shaibu aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo amerudishwa katika nafasi hiyo kwa muda kuwaongoza Super Eagles katika mechi dhidi ya Congo na Afrika Kusini wakati mchakato wa kumtafuta kocha mwingine ukiendelea.
Hata hivyo chama hicho kimesema kitampa uchaguzi kocha Keshi wa kupanga program yeyote ya mpira wa miguu ambayo kitakuwa tayari kuigharamia kwa maendeleo ya soka la Nigeria na heshima kwake kama shujaa wa taifa.
Kocha Stephen Keshi aliiongoza Nigeria kuchukua kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, na kuwa mchezaji wa pili kushinda kombe hilo akiwa kama mchezaji na baadaye kama kocha.
0 comments:
Post a Comment