EPL: WEST HAM YAICHAPA MAN CITY 2-1; LIVERPOOL YABANWA, ARSENAL YASHINDA


Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea leo michezo sita katika viwanja tofauti tofauti.Watu wameshangazwa kuona timu ya West Ham United kuzidi kufanya vizuri msimu huu na kupanda mpaka nafasi ya 4 katika msimamo baada ya kuichapa Manchester City kwa mabao 2-1 wakiwa katika uwanja wa nyumbani kwao.
Mabao ya West Ham yalipachikwa na Morgan Amalfitano katika dakika ya 21 kabla ya Diafra Sakho kuandika bao la pili katika dakika ya 75.Bao la kufutia Machozi la Manchester City lilipachikwa na David Silva kunako dakika ya 77.
Matokeo ya michezo mingine ni Liverpool 0-0 Hully City,Southampton 1-0 Stoke City,Sunderland 0-2 Arsenal,West Bromich 2-2 Crystal Palace na Swansea City 2-0 Leicester City.

0 comments:

Post a Comment