Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika
kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la
polisi la nchi hiyo limesema.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando
Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika
mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.
Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.
Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.
Mashirikisho la Soka la Kimataifa
(Fifa) na lile la Africa (Caf) yametuma salamu la rambirambi kutokana na kifo
cha nahodha wa Afrika Kusini, Bafana Bafana Senzo Mayiwa.
0 comments:
Post a Comment