Maelfu ya mashabiki nchini Afrika Kusini wamehudhuria maombolezi ya
kipenzi chao kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini Senzo Meyiwa
aliyepigwa risasi siku ya Jumapili na watu wasiojulikana.Maombolezi hayo
yaliyofanyika kwenye uwanja wa Standard Bank Arena jana pia
walijumuishwa kwenye maombolezi hayo wanamichezo wengine wawili
waliofariki ndani ya wiki hii ambao ni mkimbiaji wa zamani wa mita 800
Mbulaeni Mulaudzi aliyefariki kwa ajali ya gari na pia bondia wa kike
Phindile Mwelase.`Katika sherehe hiyo ya kuomboleza wanamichezo wa
Afrika Kusini pia walikuwepo watu maarufu kama nahonda wa timu ya Rugby
Jean de Villiers,Winnie Mandela na wengineo wengi.
Waombolezaji wakiimba kwa nyimbo kama njia ya kuwakumbuka wapendwa wao Senzo Meyiwa,Mbulaeni Mulaudzi na Phindile Mwelase |
0 comments:
Post a Comment