CHELSEA YAIVURUGA LIVERPOOL: DIEGO COSTA SHUJAA


Chelsea imeendelea kuonyesha ina kikosi bora baada ya kuitwanga Liverpool kwao Anfield kwa mabao 2-1.
Shujaa katika Mechi ya Ligi Kuu England ni Mhispania, Diego Costa ambaye alifunga bao la pili katika dakika ya 67.
Hadi mapumziko, Liverpool na wageni Chelsea sasa ni mapumziko na matokeo ni 1-1.



Liverpool walianza kupata bao kupitia Emre Can kwa shuti kali katika dakika ya 9 likiwa ni bao la haraka au mapema zaidi kwa msimu huu kwa Liverpool.

Chelsea wakasawazisha katika dakika ya 14 mfungaji akiwa Gary Cahill.
Kipindi cha kwanza Liverpool ndiyo walimiliki mpira zaidi, lakini Chelsea wakafanya mashambulizi mengi zaidi na mchezaji pekee aliyepewa kadi ya njano katika kipindi hicho ni ni Rahim Sterling baada ya kumfanyia madhambi Ramirez.











0 comments:

Post a Comment