PREVIEW YA MECHI ZA LEOLIGI KUU BARA: YANGA VS MGAMBOA, KAGERA VS MTIBWA,


Match Preview: Yanga – Mgambo, Wenyeji wanakibarua kizito kurudisha heshima
 Ligi kuu Tanzania bara inaendelea leo kwa mechi tano katika viwanja tofauti, ambapo mabingwa watetezi timu ya Azam, Yanga na wengineo watajitupa uwanjani usaka pointi tatu muhimu.

AZAM VS COASTAL UNION; Mchezo huu utachezwa katika uwanja wa Chamazi, ambao ni nyumbani kwa Azam Fc.Huu ni mchezo mgumu ambapo Azam, mabingwa watetezi watakuwa na hamu ya kurudisha heshima yao baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Ndanda na Ruvu Stars, Kwa Upande wao Coastal Union watakuwa na moto wa kuendeleza wimbi la ushindi hasa baada ya ushindi wao dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi iliyopita,

YANGA VS JKT MGAMBO: Huu pia utakuwa ni moja ya michezo yenye ushindani hasa kutokana na ubora wa timu zote mbili, ambapo licha ya Yanga kuwa na jina kubwa na kuwa mwenyeji wa mchezo huo itategemea upinzani kutoka kwa Mgambo ambayo imeonekana kuamka baada ya kupoteza michezo mitatu ya awali na kushinda michezo miwili mfululizo katika mechi zake za mwisho kabla ya kesho,Yanga kwa upande wao pia watakuwa na machungu ya kupunguza baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar walichoipata mwishoni mwa wiki iliyopita.

 Yanga wanashikilia nafasi ya nne wakiwa na pointi 10 huku Mgambo wapo nafasi ya 6 wakiwa na pointi 9 waizidiwa magoli na Kagera Sugar iliyo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 9 pia.

MTIBWA SUGAR VS KAGERA SUGAR: Huu utakuwa ni moja ya mechi ngumu zisizotabirika itakayopigwa katika uwanja wa Manungu huko Turiani Mkoani Morogoro, ambapo Mtibwa atakuwa mwenyeji,Ambapo timu zote hazijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi tano zilizokwisha kucheza.Mtibwa katika michezo mitano\ imeshinda michezo 3 na kutoa sare mechi 2, huku Kagera wao wakiwa kinyume na Mtibwa kwa kushinda michezo 2 na kutoka sare michezo 3.

MICHEZO MINGINE

STAND UNITED VS MBEYA CITY 
Uwanja: Kambarage Stadium(Shinyanga)

POLISI MOROGORO VS TANZANIA PRISONS.
Uwanja: Jamhuri Stadium(Morogoro)
 

0 comments:

Post a Comment