KOCHA wa zamani wa Simba Patrick Liewig anatarajia kutua nchini
Novemba 17, baada ya kumalizana na uongozi wa Azam kwa ajili ya kuongeza
nguvu katika benchi lake la ufundi lililo chini ya kocha Mcameroon
Joseph Maurus Omog.
Habari kutoka kwa mmoja wa
viongozi wa Azam zinasema wameona ni vyema kocha huyo akaja hivi sasa
kusaidiana na Omgo baada ya kuondokewa na makocha wawili Kali Ongala na
Vivin Nagal raia wa India.
Liewig alikuwa kocha wa Simba msimu uliopita. Lakini uongozi wa
Ismail Aden Rage ukamuondoa na nafasi yake ukampa Abdallah Kibadeni
ambaye hata hivyo hakudumu zaidi ya nusu msimu.
0 comments:
Post a Comment