Bao pekee la Karim Benzema limeipatia Real Madrid ushindi wa pili mfululizo dhidi ya Liverpool hapo jana usiku katika uwanja wa Bernabeu.
Mfaransa huyo aliifungia timu yake goli hilo katika dakika ya 27 ya mchezo, ambao ulishuhudia nyota wengi wa Liverpool wakipumzishwa, akiwemo Balotelli, huku Gerald na Sterling wakitokea benchi.
Hata hivyo Madrid watajilaumu kwa kukosa nafasi nyingi za wazi hasa kupitia kwa nyota wake Ronaldo.
0 comments:
Post a Comment