KINDA
Brooklyn Beckham ameripotiwa kusaini Mkataba wa kujiunga na akademi ya
Arsenal licha ya Chelsea na klabu ya zamani ya baba yake, David,
Manchester United kumtaka pia.
Mtoto
huyo mkubwa wa Nahodha wa zamani wa England alitakiwa na klabu kadhaa
za Ligi Kuu ya England, lakini kinda huyo wa umri wa miaka 15
inafahamika amechagua Arsenal baada ya kuwavutia makocha Kaskazini mwa
London.
Brooklyn
amekuwa akifanya mazoezi na The Gunners na kuchezea kikosi cha vijana
chini ya umri wa miaka 16, baada ya awali kuchezea Chelsea, United,
Queens Park Rangers na Fulham.
Brooklyn ni mtoto mkubwa wa Nahodha wa zamani wa England, David Beckham
0 comments:
Post a Comment