Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari kimewasili
Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa maandalizi ya mechi dhidi ya
Swaziland uliopo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA).
Mechi hiyo itafanyika Jumapili (Novemba 16 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa wa Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa
itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha Mart Nooij wapo kwenye msafara huo
isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye amebaki Dar es Salaam
kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Credits:Hivisasa Web.
0 comments:
Post a Comment